Aveline Joseph

0 Min 0 Participants
Kipenyo cha Duara
"KIPENYO CHA DUARA" Wanafunzi wagawanyike katika makundi ya watu 5. Mwalimu waambie wanafunzi waandae mifuniko ya ndoo na mifuniko ya makopo ya maji,uzi na rula yenye vipimo. Katika kila kundi wapime urefu wa mfuniko wa ndoo au kopo kwa kugawa nusu kwa nusu kwa kutumia uzi kisha ule urefu wa uzi upimwe katika rula na kubainisha urefu uliopatikana. Kisha waulize wanafunzi wataje hilo ni umbo gani? lililopimwa na pia urefu huo katika umbo hilo unaitwaje? Katika somo la hisabati? na kisha wawasilishe mbele ya darasa. -hii inafaa kwa somo la Hisabati. -na pia kazi hii inafaa kwa darasa la 6 na 7 -stadi zingine ambazo zinapatikana katika kazi hii stadi ya kuwasiliana, kushirikiana, kufikiri, kujitambua

Comments

avatar
blessings Rweikiza
2 years ago

good